Wanaomchukia Harmonize hawajui mziki,ni muandishi bora(Video)
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia video mpya ya Harmonize ya SIDE aliyowashirikisha KJ Spio na Libianca
Anasema kuwa Harmonize kuna namna amebadilika baada ya kutoa Album iliyobuma ya Muziki wa Samia, sasa ameamua afanye muziki wa kumalizia mwaka.
Anaongeza kuwa baada ya album hiyo kubuma kuna namna Harmonize ameachia ngoma kadhaa na zimekuwa na ubora mkubwa sana kwenye upande wa Uandishi.
Kingine melody za ngoma hizo zimekuwa kivutio kwa wengi hata challenge mashabiki wamezifanyia sana, ametoa mfano ngoma kama Disconnect, Ujana/Yanga Bingwa na You Better Go.
Anasema kuna watu wengi wanamchukia Harmonize bila sababu lakini jamaa anazalisha muziki mkubwa sana Consistently labda kwa sababu mashabiki wameamua kuchagua pande zao na sio muziki mzuri.
Anaongeza Harmonize ana mapungufu yake kama wengine lakini lifanya jambo zuri apongezwe pia, kufanya Collabo na Libianca sio kitu rahisi.
Anachokitengeneza Harmonize matokeo yake hayawezi kuonekana leo wala kesho ila kuna muda yataonekana tu.