Promotion

Wanaotaka kununua ving’amuzi vya DStv na wamepungukiwa hela, Kuongezewa mkwanja bure (+video)

Miezi michache baada ya fanyika kwa tamasha kubwa la filamu Zanziba (ZIFF) DStv imetangaza kufungua chaneli
maalum (pop-up Channel) kwa muda wa siku mbili ili kuweza kuonyesha filamu mbalimbali zilizofanya vizuri katika
tamasha hilo.

Katikati ni Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo na Kushoto ni Mchekeshaji Mr. Beneficial .

Filamu hizo ni kutoka katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, Kenya, Afrika Kusini, Marekani, Iran,
Morocco, Nigeria, Cape Verde na Zimbabwe.

Chaneli hiyo itakuwa DStv 197 na itakuwa wazi kwa siku mbili Jumapili 29 Septemba na Jumatatu 30 Septemba
kuanzia saa 12 Jioni hadi saa 4:30 Usiku.

Miongoni mwa filamu hizo zitakazoonyeshwa ni pamoja na filamu maarufu ya SEMA ambayo imewahusisha
waigizaji na wachekeshaji maarufu nchini Timamu (Mr. Beneficial, Bwana Mjeshi, Ebitoke, Onestory Kweka)
ambayo inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kutokana na ubora wake na umaarufu wa waigizaji hao. Filamu hiyo ya
SEMA itaonyeshwa siku ya Jumapili 29 Septemba kuanzia saa 4 usiku.

Akizungumzia uamuzi wa DStv kufungua chaneli maalum kuonyesha filamu hizo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice
Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa unalenga kulitangaza Zaidi tamasha la ZIFF pamoja na kuwapa watu
ambao hawakuweza kuhudhuria tamasha hilo fursa ya kuona filamu mbalimbali zilizoonyeshwa.

Hii ni fursa kwa watu kuona yaliyojiri ZIFF na tunafurahi kuwa mbali na kwamba kulikuwa na filamu kutoka mataifa
mbalimbali ulimwenguni, filamu zetu za Tanzania pia zilifanya vizuri kwenye tamasha hilo. ZIFF ni moja ya
matamasha yanayoitangaza nchi yetu kote duniani hivyo na sisi kama vinara wa kutoa burudani tumeona ni vyema
watu wapate uhundo huo kupitia chaneli yetu hii maalum itakayopatikana kwenye vifurushi vyote vya DStv kuanzia
kile cha DStv Bomba kwa sh.19, 000 tu, kwa mwezi.” – amesema Shelukindo.

Naye muigizaji wa filamu ya SEMA, Brian Anaeli Mrikaria maarufu kama ‘Mr. Beneficial’ amesema kuonyeshwa kwa
filamu yao katika chaneli hiyo maalum ya DStv ni kitu cha kujivunia kwani pia itasaidia kuonyesha kuwa Tanzania
tuna vipaji na tunaweza kufanya vitu vyenye viwango vya kimataifa.

Kutokana na fursa hiyo, Mr. Beneficial amesema kuwa yeye na Bosi wake watawaongezea hela watu 10 ambao watakuwa wamepungungiwa fedha za kununua king’amuzi cha DStv.

Tamasha la ZIFF ni moja ya matamasha makubwa ya filamu hapa Afrika na hufanyika visiwani Zanzibar kila mwaka.
Tamasha hili limekuwa likifanyika kwa Zaidi ya miaka 20 sasa na linazidi kuwa maarufu huku kukiwa na washiriki

Related Articles

Back to top button