Wanaotikisa usajili Ulaya, dau la Jadon Sancho kwa Manchester United

Manchester United haitalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho.

Jadon Sancho wants to return to the Premier League with Man Utd ...

Hatahivyo, klabu hiyo ya Bundesliga inataka ongezeko la pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)Arsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huuArsenal wanafikiria kumtumia Matteo Guendouzi kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu

Arsenal wanafikiria kumtumia kiungo wa kati Matteo Guendouzi, 21, kama sehemu ya mpango wowote wa kubadilishana msimu huu. (Mail)

Tottenham wanaamini kuwa watampata kiungo wa Southampton Pierre-Emile Hojbjerg,24, msimu huu lakini watapaswa kuwauza wachezaji kwanza. (Telegraph)Manchester United wanafikiria kumchukua Nathan Ake

Manchester City wana mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Bournemouth Nathan Ake, 25. Hatahivyo wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea, ambao wanamtaka mchezaji huyo pia. (Athletic)

Beki wa kulia wa Barcelona Marc Jurado,16, ameondoka katika klabu ya Catalan. Mhispania huyo anajiandaa kujiunga na Manchester United msimu huu(ESPN)Juventus wanamsaka winga Mhispania anayechezea Valencia, Ferran Torres

Juventus wanamsaka winga Mhispania anayechezea Valencia, Ferran Torres

Juventus imeongeza ushawishi wao kwa winga Mhispania anayechezea Valencia Ferran Torres,20. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United na Borussia Dortmund. ( Mail via Onda Cero)

Manchester City imekubali kumuuza winga Leroy Sane kwa Bayern Munich mchakato utakaowaingizia kiasi cha pauni milioni 54.Manchester City imemuachilia Leroy SaneMchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21,ameonekana Italia kabla ya uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Inter Milan. (Mail)

Roma imethibitisha kuwa mkopo wa Henrikh Mkhitaryan kutoka Arsenal umeongezwa mpaka mwishoni mwa msimu. Mchezaji huyo, 31, anayecheza nafasi ya kiungo wa kati alijiunga na timu hiyo ya Serie A mwezi Septemba. (Evening Standard)

Related Articles

Back to top button