Habari
Wanawake na Vijana kuwezeshwa kwenye Kilimo

TADB imesaini makubaliano ya ushirikiano na Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kwa lengo la kuwawezesha wanawake na vijana waliopo katika minyororo ya thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Kupitia makubaliano hayo, pande hizo zitashirikiana kufanya tafiti juu ya mahitaji ya wanawake, kutoa mafunzo ya ujuzi, kupanua fursa za mikopo, pamoja na msaada wa kitaalamu katika usimamizi wa biashara na matumizi ya teknolojia.
Dkt. Mwajuma Hamza wa TWCC amesema makubaliano hayo yataondoa vikwazo vya wanawake katika biashara za kilimo, huku Bi. Adolphina William wa TADB akisisitiza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa huduma za kifedha zenye kugusa moja kwa moja walengwa wa sekta hiyo.