Bongo5 ExclusivesHabariMahojiano

Wanawake na wasichana watoa tamko kuhusu mabadiliko ya sheria ya ndoa za Utoto

Wakizungumza na wana habari TAPO la Wanawake na wasichana kwa kutambua tamko alilotoa Bungeni siku ya jamanne ya tarehe 13 september 2022, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalumu Dr. Dorothy Gwajima alipoliambia Bunge na wananchi akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu CCM Amina Daud Hassan alisema kuwa:

“Wiki ijayo kamati ya maendeleo ya jamii pamoja na kamati ya sheria na katiba zitaketi kwenye kikao kwa ajili ya kufanya marekebisho ya sheria ya ndoa, hivyo basi tumepokea hoja yake tunaenda kuiwasilisha na kujuisha ili vijadiliwe kwa pamoja”

Mbali na hilo wamempongeza Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson aliposema kuwa:

“Binafsi miaka 18 bado sio umri sahihi kwa watoto kuozwa, binafsi siwezi kumruhusu binti yangu kuolewa katika umri wa miaka 18 kwani umri huo binti hawezi kumudu majukumu ya ndoa anapaswa awe shule anasoma elimu ya juu” Dr. Tulia Ackson alisema maneno hayo wiki iliyopita akiwa Dodoma na kuripotiwa na gazeti la The Citizen

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents