Wanawake wanywe Alikasusi haina madhara, wengi wanaiogopa ni kahawa tu – Mtaalamu
Mtaalamu anayetegeneza na kuuza kinywaji kinachoitwa Alikasusi amefunguka juu ya Kinywaji hicho ambacho watu wengi wanaamini kuwa kinaongeza nguvu za Kiume.
Akiongea na @el_mando_tz mtaalamu huyo amesema kuwa kinywaji hicho ni kahawa iliyotengenezwa kwa kuchanganywa na miti mbalimbali na imetengenezwa maalumu kwa lengo la kusisimua mwili.
Ameongelea kuhusu watu wengi kuamini kuwa kinywaji(Kahawa ) hiyo inaongeza nguvu za kiume, mtaalamu huyo amekanusha na kusema kuwa wanaouza Alikasusi na kuwaambia watu inaogeza nnguvu za kiume huwa kuna kitu wanachanganya ila kiuhalisia haitibu tatizo hilo.
Baada ya kuulizwa kuwa kwa upande wa wanawake vipi au inatakiwa kutumiwa na wanaume tu amedai kuwa Alikasusi inatumiwa na watu wote haichagui jinsia.
Kwako unaamini vipi?? Alikasusi watu wanakuywa kwa lengo gani??