Habari

Wanigeria marufuku kuingia Dubai, nchi hizi zapewa nafasi

Baada ya UAE kutangaza kufungia visa raia wa nigeria October 2022, bodi ya utalii ya Dubai imehamishia nguvu yao kwa nchi nyengine za Afrika kama Tanzania, Kenya, South Africa na kutambulisha mabalozi wanaowakilisja nchi hizo akiwemo msanii wa South Africa Thabsie na msanii kutoka Kenya Bahati. Hata hivyo bodi ya utalii Dubai inaendelea kutafuta mabalozi wa kuwakilisha nchi hizo katika kutalii Dubai.

Mabalozi hao wanategemewa kutumia umaarufu wao kuonesha watu wa nchi zao vitu ambavyo vinapatikana Dubai ili kuwavutia na wamejiunga na kampeni inayoitwa A to Z of Dubai inayoonesha watalii vitu vizuri vya Dubai.

Ripoti zinaeleza pia kwamba aliekua rais wa Nigeria Muhammad Buhari ameomba Dubai waondoshe kuwafungia kwa visa wanaijeria na kuonesha utayari wa kuzungumza juu ya tofauti zao na kuweza kuwakaribishia wanaijeria nchini humo tena.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents