Bongo5 MakalaHabariMakalaMichezo

Brazil wanaitambua Uhispani taifa la Kibaguzi – Vinicius Jr

Siku ya Jumapili katika mchezo kati ya Valencia na Real Madrid zote kutoka nchini Uhispani ulipigwa katika dimba la Mestalla linalomilikiwa na klabu ya Valencia.

Katika mchezo huo ambao Real Madrid walipoteza kwa kufungwa goli moja uligubikwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi kwa winga wa real Madrid na taifa la Brazil Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior alimaarufu kama Vinícius Jr mwenye umri wa miaka 22.

Vitendo hivyo vya kibaguzi vilimtoa kwenye mchezo Vini hadi kupelekea kubishana na mashabiki waliokuwa wakimuita Mono kwa lugha ya Kihispani lakini likimaanisha Monkey au Nyani.

Licha ya kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya mvutano kati yake na mlinda mlango wa Valencia Giorgi Mamardashvili baada ya refa kutafsiri kuwa alimpiga kofi mchezaji wa Valencia licha ya yeye kukabwa shingo na  wachezaji wa Valencia.

Baada ya sakata hilo imeelezwa kuwa mwendesha VAR ambaye alitoa maamuzi Vini kupewa kadi nyekundi amesimamishwa kazi kwani imeelezwa ilitolewa kimakosa na kwa kuegemea upande mmoja.

Licha ya hilo lakini pia La liga imewakamata mashabiki wanne ambao walionekana kwenye kamera wakimbagua Vini Jr igawa karibia uwanja mzima ulikuwa ukiimba ‘Mono’

Wanaharakati wengi na wachezaji mbalimbali dunniani wameonyesha kukerwa na vitendo hivyo na kuamua kuvipigia kelele na kupinga.

Moja ya kauli nzito aliyoitoa Vinicius ni kwamba Taifa la Brazil linalichukilia taifa la Uhispani kama taifa la Kibaguzi zaidi na pia wannaichukulia ligi ya Uhispani La Liga kama ligi ya Kibaguzi zaidi.

Kauli hiyo umeungwa mkono na wadau mbalimbali wakieleza na kuweka matukio yakiwemo ya Akina Etoo walivyokuwa wanabaguliwa Uwanja bila uamuzi wowote kuchukuliwa.

Vinni amepost video hii akionyesha namna mashabiki wa vilabu karibia vyote Uhispania wanavyombagua kwa rangi yake wakimuita Nyani. There’s No Room for Racism.#sayNotoRacism✊🏿 #KemeaUbaguziWaRangi

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents