BurudaniMuzikiVideos

Wasanii wa Sony Music kukaa muda mrefu bila kuachia project kuna athari?

Ni good news hivi karibuni RockStar 4000 pamoja na Sony Music kutangaza kumsaini rapa anayechikupia kwa kasi zaidi nchini Tanzania @YoungLunya ambaye alishinda tuzo mbili, Msanii bora wa Hiphop na wimbo bora wa hiphop ‘Mbuzi’ kupitia Tanzania Music Award (TMA).

Rockstar 4000 / Sony Music Africa wamefanya kazi na wasanii wengi wa Tanzania akiwemo Alikiba, Rose Mhando, Ommy Dimpoz pamoja na Barakah Da Prince.

Ni ndoto ya kila msanii kuaminika na kupata lebo kubwa yenye uwezo wa kusimamia vipaji vyao ili kutimiza ndoto zao, na ndio maana baada ya rapa huyo kutangazwa na lebo hiyo kubwa Afrika kila mtu alipongeza juhudi hizo huku wengi wakitarajia kuona makubwa kutoka kipaji hicho kichanga.

Wadau wa muziki bado wana mashaka kutokana na historia yenye kutia mashaka kwa wasanii waliopita katika lebo ya RockStar na Sony Music huku ikishindwa kueleweka kama tatizo lipo upande wa lebo au kwa wasanii wetu.

Wasanii waliowahi kupita katika lebo hiyo ni pamoja na Alikiba, Rose Muhando, Ommy Dimpoz pamoja na Barakah Da Prince.

Alikiba

Ni ambaye kwa sasa yupo chini ya lebo yake King Music, alikaa RockStar kwa miaka mingi na baadae kuwa mshirika wa kampuni hiyo kwa upande wa Afrika Mashariki. Lakini baade aliachana lebo hiyo.

Moja ya mabadiliko makubwa ya Alikiba wa RockStar, na huyu wa sasa ni jinsi anavyoachia project.

Moja ya kelele kubwa ambazo zilipigwa akiwa na lebo hiyo ni mtindo wakuachia ngoma, ucheleweshwaji. Kuna wakati mpaka mashabiki wakawa wanachukizwa na tibia hiyo huku wengine wakitangaza kuhamia kwa Diamond.

Alikiba wa sasa ni mwingine kabisa, anatoa dozi bila hata mgonjwa kuombwa, huwenda aliona tatizo katika lebo yake iliyopita.

Rose Mhando.
Huyu ni miongoni mwa wasanii waliokaa muda mrefu RockStar kwa mafanikio makubwa ingawa alipitia mtindo huyo huyo wa kuachia ngoma.

Muimbaji huyo pendwa wa Injili alikaa zaidi ya miaka miwili katika lebo hiyo bila kuachia project yoyote.

Katika moja na mahojiano yetu na Seven Mosha kipindi wanamtangaza msanii huyo rasmi baada ya miaka miwili ya kumsaini, aliiambia Bongo5 exclusively kuwa mwishoni mwa mwaka huu (2013) kazi mpya za Rose Muhando zitaanza kutoka. Amesema kwa kipindi chote hicho, Rose Muhando alikuwa akirekodi nyimbo mpya kwenye studio za Sony Music Afrika zilizopo nchini Afrika Kusini.

Muimbaji huyo aliachana na lebo hiyo vizuri na kusema ulimfungulia dunia kwa mambo mengi mazuri huku adai katika mtindo wa kuachia nyimbo ndio kuna changamoto kwa sababu kunakuwa na foleni.

Changamoto ya mtindo wa kuachia ngoma kwa wakati imekuwa ikitajwa
kupitia lebo hiyo, ingawa Rose Muhando alisema hali hiyo haikuathiri muziki wake labda ni kutokana na aina ya muziki wa Injili anaofanya, Je kwenye BongoFleva msanii anaweka kukaa miaka miwili au mmoja bila wimbo na brand yake itakuwa sawa?

Kila la heri Young Lunya, bado mashabiki wana kiu kubwa na muziki wako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents