Burudani

Wasanii waliopigwa rungu na BASATA walegezewa

Kikao cha kusikiliza rufaa ya Wanamuziki wa bongofleva chini @whozu_@_bilnass_official na @mbosso_ kimefikia maamuzi ya kuwataka wasani hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa chini kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao chini ya uongozi wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro kilichofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dares salaam ambapo Mwanamuziki @whozu_ anatakiwa kulipa faini.

Naye @bilnass_official na @mbosso_ wameondolewa adhabu za kufungiwa.

Aidha msanii Whozu amepewa masaa sita ili kutekeleza azimio la kushusha wimbo huo kwene
“digital platforms” zote kama makubaliano yanavyoelekeza.

Mhe. Waziri amewahasa wasani hao na wengine nchini kutumia ubunifu kwa kufuata taratibu ulioainishwa katika mongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents