Habari

Washiriki Wa Mbio Za Tigo Kilimanjaro International Half Marathon Watakavyohudumiwa

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akizungumza na Waandishi wa Habari, namna walivyojipanga kuwahudumia wateja wa Tigo watakaoshiriki mbio za Kilimanjaro International Half Marathon zinazodhaminiwa na Tigo zitafanyika Februari 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Kilimanjaro, Moshi 20 Februari 2024: Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo ambao ndiyo wadhamini wa mbio za Tigo Kilimanjaro International Half Marathon Km 21 wameelezea jinsi walivyojipanga kuwahudumia washiriki wa mbio hiyo.

Akizungumza na Wanahabari Mjini Moshi Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema; “Tukumbuke kuwa Tigo tunaongoza mapinduzi ya kidigitali hapa Tanzania.
“Na ili kuendelea kuwa viongozi katika sekta hii, uwekezaji kwenye miundombinu ya mawasiliano ni jambo la muhimu sana. Kuanzia mwaka 2022, Tigo tumewekeza zaidi ya shilingi trilioni 1, ili kuboresha miundombinu yetu ambapo tunategemea hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2024, tutakuwa na teknolojia ya 4G nchi nzima na 5G katika miji mikubwa.
“Uwekezaji huu umetupatia tuzo ya kimataifa ambapo Tigo tumethibitishwa na Ookla, kama mtandao wenye kasi zaidi

Tanzania. Pia kupitia ripoti ya robo ya mwisho ya mwaka jana, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imethibitisha kuwa Tigo ni mtandao wenye huduma bora zaidi Tanzania (Quality of Service).

Vile vile, Tigo tutakuwa na Wi-Fi spots (Bure 4G) katika sehemu mbalimbali hapa Mjini Moshi, Bar Amuz, Redstone, Moshi Pazuri, Kili Home pamoja na Moshi Club ambapo ndio tamasha kubwa la Tigo Kili-Half International Marathon 2024 litafanyika.

Kwa niaba ya Kampuni ya Tigo, naomba kuwaalika wageni wote Mjini Moshi kujiunga nasi kwenye Kilimanjaro International Marathon hususani Tigo Kili- Half International Marathon.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents