Habari

Wasiochanjwa kuzuiwa kuingia katika sehemu za biashara Ujerumani

Viongozi wa Ujerumani wameidhinisha vizingiti vipya vya COVID kwa watu ambao hawajachanjwa ambao watakabiliwa na vikwazo zaidi baada ya viongozi wa Ujerumani kufanya mazungumzo siku ya Alhamisi.

Kansela wa Ujerumani anayeondoka Angela Merkel

Kansela anayemaliza muda wake wa Ujerumani Angela Merkel na Kansela mteule Olaf Scholz walizungumza na viongozi wa majimbo yote 16 nchini Ujerumani na kukubaliana juu ya hatua mpya za kupunguza ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya corona.

Watu ambao hawajachanjwa watazuiwa kuingia kwenye sehemu za biashara karibu zote, isipokuwa kwenye maduka ya chakula na ya dawa. Kansela anayeondoka Angela Merkel ameserma anamuunga mkono kansela mteule Olaf Scholz katika hatua yake ya kutaka chanjo ziwe ni lazima.

Yapi yaliyopitishwa na viongozi?

Viongozi wa shirikisho na serikali za majimbo walikubaliana yafuatayo:

  • Ni watu waliopewa chanjo tu au waliokwisha ugua COVID-19 na kupona ndio watakaokubaliwa kuingia kwenye maduka ya bidhaa zisizo za lazima kama ya nguo na kadhalika, migahawa, majumba ya makumbusho, kumbi za sinema.
  • Vipimo vya ziada kwa waliochanjwa.
  • Bunge kupiga kura mapema mwaka 20222 kuhusu swala la chanjo kuwa ni lazima.
  • Vilabu vya usiku, kumbi za muziki zitafungwa katika maeneo ambayo kiwango cha maambukizi kitafikia watu 350 na zaidi.
  • Hatua hizo mpya kuanza kutumika mara tu zitakapoidhinishwa na wabunge, yumkini katika siku chache zijazo.
  • Watazamaji wasiozidi 15,000 wataruhusiwa katika viwanja vya soka.
  • Viwanja vya michezo vya ndani vitahudhuriwa na watu wasiozidi 5,000.
  • Mikusanyiko ya faragha kwa watu ambao hawajachanjwa wataruhusiwa watu wa kaya moja pekee.
  • Wanafunzi watahitaji kuvaa barakoa wakiwa shuleni.

Huku kirusi kipya cha omicron kikiongeza hofu ya kuzorota kwa hali ambayo tayari ni mbaya nchini Ujerumani na hospitali za nchi hiyo zikiwa zimejaa wagonjwa wa COVID-19, bibi Merkel amesema hali ni mbaya sana licha ya maambukizi kupungua lakini kiwango bado ni cha juu sana.

Kansela wa Ujerumani mteule Olaf ScholzKansela wa Ujerumani mteule Olaf Scholz

Hadi kufikia sasa ni chini ya asilimia 69 tu ya wakazi wa Ujerumani ambao wamechanjwa kikamilifu hii ikiwa ni idadi ndogo ya watu waliopokea chanjo katika nchi za Ulaya Magharibi.

Madaktari wa magonjwa ya kuambukiza wamesema ongezeko la maambukizi linatokana na ukinzani wa kupata chanjo  kwa watu sehemu kubwa ya watu walio na mashaka na chanjo hizo miongoni mwa jamii.

Je, hali ya janga la corona ikoje nchini Ujerumani?

Ujerumani imeshuhudia ongezeko la watu wanaoambukizwa virusi vya corona huku wanasayansi na wataalamu wa afya wakiikosoa serikali kwa kuchelewa mno kuchukua hatua. Mkuu wa chama cha wahudumu wa wagonjwa mahututi DIVI nchini Ujerumani amesema huenda hadi watu 6,000 wanaweza kulazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi kufikia Krismasi.

Chanzo DW

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents