Wataka kumuondoa Rais kwa kuitangaza sarafu ya $LIBRA kwenye mtandao wa X

Rais wa Argentina, Javier Milei, anakabiliwa na wito wa kuondolewa madarakani pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na uhamasishaji wake wa sarafu ya kijigitali (cryptocurrency) kwenye mitandao ya kijamii.
Milei alichapisha kwenye X, awali Twitter, kuhusu sarafu ya $LIBRA Ijumaa, akiwa ameeleza kwamba itasaidia kufadhili biashara ndogo ndogo na kampuni changa.
Akatoa mpaka na njia ya namna ya kununua sarafu hiyo, jambo hilo lilisababisha bei yake kupanda ghafla. Lakini ndani ya masaa machache, alifuta chapisho hilo na thamani ya sarafu hiyo ikaporomoka, na hivyo wawekezaji kupoteza sehemu kubwa ya fedha zao.
Baadhi ya wanasiasa wa upinzani katika Bunge wanasema wanapanga kuanzisha taratibu za kumuondoa madarakani Milei, huku mawakili wakisema wamewasilisha malalamiko ya ulaghai katika mahakama ya jinai ya Argentina Jumapili.
Watu wengine mtandaoni wamemlaumu Milei kwa kitendo kinachojulikana kama “rug pull,” ambapo waendelezaji wa safaru za mtandaoni huvutia wanunuzi, kisha kusitisha shughuli za biashara na kutoboa fedha zilizokusanywa kutokana na mauzo.
Waliongeleza kuwa kiunganisho (link) kilichotumika kununua sarafu hicho kilikuwa na maneno ambayo rais hutumia katika hotuba zake.
Hata hivyo, ofisi ya rais ya Argentina ilisema Jumamosi kuwa uamuzi wa kufuta chapisho huo ulikuwa wa kuzuia minong’no kufuatia mwitikio wa umma juu ya alichokifanya. Taarifa hiyo ilisema Milei hakuwa amehusika katika maendeleo ya cryptocurrency, na kwamba Ofisi ya kupambana na Rushwa ya serikali itachunguza na kuamua kama kuna yeyote aliyefanya makosa, ikiwa ni pamoja na rais mwenyewe.
Wapinzani wa kisiasa wa Milei wametumia fursa hii kumkosoa. Rais wa zamani, Cristina Fernández de Kirchner, ambaye kwa sasa yuko upande wa upinzani, alimkosoa vikali akimwita “mdanganyifu wa crypto” katika chapisho lililotazamwa mara 6.4 milioni.
Kwa upande wake, muungano mkuu wa upinzani wa nchini homo ulisema utawasilisha ombi la kumuondoa madarakani rais huyo. Pia, Esteban Paulón, mwanachama wa Chama cha Waisocialisti cha upinzani, alisema katika chapisho kwenye mtandao wa X kwamba naye atawasilisha ombi la kuanzisha taratibu za kuondolewa madaraka.