Watanzania wahamasishwa kumuenzi Nyerere hivi

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya baba wa Taifa, Hayati Julius K Nyerere, Oktoba 14, watanzania wamehamasishwa kuweka utamaduni wa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Nyerere  ambayo ndiyo Mbuga kubwa Afrika na yenye vivutio vingi zaidi.

Afisa Mwandamizi Seti Mihayo

Hamasa hiyo imetolewa na Afisa Mwandamizi Seti Mihayo, ambapo ameeleza kuwa kutembelea hifadhi hiyo yenye historia kubwa itakuwa ni sehemu moja wapo ya kumuenzi Hayati Mwl. Nyerere.

Mhifadhi Mihayo ameeleza kwamba licha ya Hifadi ya Taifa ya Nyerere kuwa kubwa na vivutio vingi lakini pia  Hifadhi inajulikana kama moja ya eneo la urithi wa Dunia.

Mbali na kuorodhesha vivutio mbalimbali, Bw. Mihayo ameeleza kuwa Hifadhi ya Nyerere ndio yenye historia ya vita vya kwanza vya dunia pamoja na ile Majimaji na meneo mengine yana historia ya misafara ya watumwa waliopita kutokea Kilwa kwenda Bagamoyo.

Hifadhi ya Nyerere rasmi imeanzishwa 2019 baada ya kumegwa kwa Pori la akiba la Seluu na eneo kubwa kubadilishwa kuwa hifadhi ya Taifa, na kupewa jina la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati, Mwl Nyerere ili kumuenzi.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button