Watanzania watakiwa kujitokeza katika Mkesha maalum kumuombea Rais Samia na Taifa

Watanzania wameombwa kujitokeza kwa wingi katika Mkesha Maalum wa kuombea taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan katika kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 ulioandaliwa na Kanisa la Heavenly Image Manifest chini ya Prophet Edmound Mystic.
Mkesha huo unaotarajia kufanyika Februari 28,mwaka huu katika ukumbi wa Ubungo Plaza utakaohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari juu ya mkesha huo wa maombi, Prophet Mystic alisema kwa Tanzania mwaka 2025 ni moja ya mwaka muhimu kwa taifa na si sawa na miaka iliyopita kutokana na tukio kubwa Uchaguzi Mkuu mwenzi Oktoba.
Alisema kanisa linanafasi ya kuweza kulibeba taifa kwa namna moja na nyingine kwa kufanya maombi hivyo kupitia maombi hayo yatahusisha pia kumuombea Rais Samia sababu yeye ni mtawala amebeba hatima kubwa ya watanzania.
Alisema hawawezi kuombea serikali wanayoitazamia pasipo kuanza na serikali waliyonayo hivyonni lazima kumuombea Rais Samia ambaye Mungu alimuweka kwenye kiti cha Urais.
“Kila aliyemtanzania ananafasi ya kusimama na kuiombea taifa la Tanzania kwa imani yake na kile Mungu atakachompa kuombea kwa sababu biblia imesema.
“Habari ya kuombea Tanzania ni suala nyeti ambalo Mungu anaenda kuikumbuka nchi na kuirehemu,kama kuna makosa tumefanya alafu tukasimama kuomba rehema kwa Tanzania Mungu anauwezo wa kufanya kitu ,maombi ni kitendo cha unyenyekevu na tunamuhitaji Mungu aingilie kati katika haya,”alisema.
Alisema Mungu aliwaagiza Februari 28 ni siku ya kutengeneza matokeo ya nchi ya Tanzania bora hivyo kuna umuhimu wa
Watanzania kusimama na kutengeneza kesho ya nchi yetu kwa maombi.” Hatuombei mtu fulani hashinde ila tunaombea yeyote aliyekusudiwa kwa mapenzi ya Mungu kuweza kuchukua kijiti mwaka ujao, bwana awe pamoja nawe.
“Tumeona mwaka jana kwa habari ya Kenya kulivyotokewa na machafuko ambapo watumishi wa Mungu walihubiri hivyo hivyo, tunaposikia unabii umetolewa na Mtumishi wa Mungu tusiutweze unabii huo,”alisisitiza.
Akizungumzia suala la Uchaguzi, Prophet Mystic alitoa rai kwa Watanzania wanaoenda kuingia katika uchaguzi kuepuka na chochote ambacho kinaweza kuhatarisha hali ya usalama kwa watanzania.
Alisema wanapaswa kutotegemea waganga wa kienyeji katika uchaguzi Mkuu unaelekea kufanyika Oktoba mwaka huu kwani kwenye biblia imeandikwa amelaaniwa yule amtegemeae mwanadamu ni vema kumtegemea Mungu.
“Msimtegemee mganga wa kienyeji kumekuwa na kitu ambacho watu hawakifahamu mganga wa kienyeji anamsaidia mwanasiasa kushinda kwa sababu ya kitu kinaitwa kusimamisha madhabahu rohoni,”alisema.
Written by Janeth Jovin