
Takribani watu 12 wamefariki dunia na mamia kujeruhiwa wakati wa mkanyagano uliyotokea katika uwanja wa mpira wa Cuscatlan nchini El Salvador.
Nchi hiyo inayopatikana Amerika ya Kati imeshuhudia tukio hilo baya kabisa wakati zilipokutana timu mbili, Alianza FC na Club Deportivo katika mchezo wa mkondo wa pili wa mchujo wa robo fainali.
Dimba la Cuscatlan ni moja ya viwanja vikubwa El Salvador na chenye uwezo wa kuingiza zaidi ya mashabiki 44,000.
Imeandikwa na @fumo255