Burudani

Watu 13 wamepoteza maisha baada ya moto kuunguza ukumbi wa starehe

Watu 13 waliuawa na wengine 41 kujeruhiwa baada ya moto kuzuka katika ukumbi wa burudani mkoa wa Chonburi uliopo kusini -mashariki mwa Thailand.

Moto ulizuka mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia Ijumaa katika klabu ya B nightspot katika wilaya ya Sattahip, polisi walisema.

Kanda za video zinayosambazwa mitandaoni zinaonyesha watu wanaokimbia klabu wakipiga mayowe, wengine nguo zao zikiwaka..

Waokoaji wanasema nyenzo zinazoweza kuwaka kwenye kuta huenda kuwa zimezidisha moto.

Ukumbi huko Chonburi, jimbo lililoko kilomita 150 (maili 90) kusini mwa Bangkok, lilikuwa jengo la ghorofa moja lenye ukubwa wa mita za mraba 4,800 (futi za mraba 51,660).

Wazima moto walipambana kwa zaidi ya saa mbili ili kudhibiti moto huo, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Miili ya wahasiriwa – wanawake wanne na wanaume tisa – ilipatikana karibu na lango na bafu.

Wengine walipatikana karibu na kibanda cha DJ. Kufikia sasa, wote waliofariki wanaaminika kuwa raia wa Thailand.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents