AfyaHabari

Watu 22 wafariki baada ya kunywa pombe yenye sumu

Takriban watu 22 wamefariki na wengine kadhaa kulazwa hospitalini nchini India baada ya kunywa pombe yenye sumu.

Vifo hivyo vilitokea katika vijiji viwili katika jimbo la mashariki la Bihar, ambapo uuzaji na unywaji wa pombe umepigwa marufuku.

Marufuku kama hiyo hutekelezwa katika majimbo kadhaa nchini India, na hivyo kupelekea ustawi wa soko haramu la pombe ya bei nafuu inayotengenezwa katika viwanda visivyodhibitiwa na ambavyo husababisha vifo vya mamia ya watu kila mwaka.

Mwezi Julai mwaka huu, watu 42 walikufa katika jimbo la magharibi la Gujarat baada ya kunywa pombe iliyotengezwa kimagendo.

Mwaka jana, takriban watu 100 walikufa katika jimbo la kaskazini la Punjab katika tukio sawa na hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents