AfyaHabari

Watu 37 wafariki kwa kunywa pombe haramu India

Watu 37 wamekufa baada ya kunywa pombe kali iliyopigwa marufuku katika jimbo la Bihar mashariki mwa India.

Familia za wahanga wamkasa huo zimesema watu kutoka vijiji kadhaa walikunywa pombe inayotengenezwa nchini humo ijulikanayo kama “Mahua” au “Desi Daru” siku ya Jumatatu kwenye harusi na hafla nyengine.

Wengi wao walilalamikia maumivu ya tumbo na kupoteza uwezo wa kuona na kuanza kutapika.

Kufikia Alhamisi watu zaidi ya 20 walikuwa wamekufa na kufikia leo Jumamosi wengine wako hospitalini katika hali mbaya.

Polisi inawashikilia zaidi ya watu 100 wanaohusishwa na utengenezaji na uuzaji wa pombe haramu katika muda wa siku tatu zilizopita, na imekamata lita 600 za pombe haramu.

Related Articles

Back to top button