Habari

Watu 5 wafariki dunia kwa ugonjwa usiojulikana, serikali yatoa tamko

Wizara ya Afya imesema imepokea taarifa za uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana mkoani Kagera katika wilaya ya Bukoba Vijijini, kata ya Maruku na Kanyangereko, vijiji vya Bulinda na Butayaibega.

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu leo akizungumza na wanahabari juu ya mlipuko wa ugonjwa usiojulikana Mkoa wa Kagera.

 

Prof. Nagu amesema kuwa jumla ya watu 7 wanasadikika walipata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi. A
Amesema kuwa watu 5 kati yao wamefariki na wengine wawili 2 wako hospitali wanaendelea na matibabu huku mwenendo wa ugonjwa huu unaashiria uwezekano kuwa ni ugonjwa wa kuambukiza.

“Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu mwenendo wa ugonjwa huu na kuchukua hatua za kudhibiti ili usisambae” amesema Prof. Tumaini Nagu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents