Habari

Watu 7 wafariki kwa ajali ya basi Geita

Watu saba wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya basi la abiria kampuni ya Sheraton lenye namba za usajili T922 ADC.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea katika kijiji cha Mwilima Kata ya Kasamwa Halmashauri ya Mji wa Geita.

Amesema, ajali imetokea leo Machi 7, 2023 majira ya saa 10 jioni na kueleza chanzo cha ajali ni kupasuka kwa tairi ya mbele ya basi hilo.

Basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mwanza kuelekea Ushirombo mkoani Geita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents