Habari

Watu 72 wapoteza maisha Afrika ya Kusini

Watu 72 wamepoteza maisha nchini Afrika Kusini kufuatia ghasia zinazoendelea kushuhudiwa kati ya wafuasi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma na maafisa wa usalama.

Kwa siku zipatazo tano,wafuasi wa  Zuma ambaye anaendelea kutumikia kifungo chake cha miezi 15 jela, wamekuwa wakiandamana katika miji mbalimbali nchini Afrika Kusini kushinikiza kuachiliwa huru kwa kiongozi wao.

Machafuko hayo yanakwenda sambaba na waandamanaji kufanya vurugu kwa kuvunja na kuvamia maduka makubwa nchini humo katika jiji la Johannesburg na mkoa wa KwaZulu-Natal.

Licha ya Rais Cyril Ramaphosa kuagiza kutumwa kwa wanajeshi zaidi ya Elfu mbili kuzuia wizi wa mali na maandamano hayo, hali inaoenekana kuendelea kuwa mbaya.

Maafisa wachache wa usalama wameoneakana karibu na maduka yanayoporowa na wananchi wa taifa hilo, huku idadi ya vifo ikiendelea kupanda,hasa kutokana na watu kukanyagana.

Watu wengine zaidi ya Elfu Moja na mia mbili wamekamatwa katika machafuko hayo.

Wafuasi wa Jacob Zuma wanasema wataendelea kuandamana hadi kiongozi wao  atakapochiliwa huru.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents