HabariSiasa

Watu milioni mbili wakumbwa na mafuriko Bangladesh

Nchini Bangladesh, zaidi ya watu milioni mbili wanaaminika kukwama nyumbani kwao kutokana na maji mengi yaliyosababishwa na mafuriko.

Eneo la Kaskazini mashariki mwa nchi hiyol imezidiwa na hali inaweza kuwa mbaya zaidi Jumamosi hii, Juni 18. Kunaripotiwa hal mbaya zaidi katika nchi hii yenye wakazi milioni 160 ilio katika hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Mwezi uliopita, mafuriko yalikumba sehemu hizi za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa Bangladesh, na kuharibu mazao, kuharibu nyumba na barabara na kuua angalau watu 12, anaripoti mwandishi wetu huko Bangalore, Côme Bastin.

Katika kujaribu kuwasaidia wakazi ambao nyumba zao zimejaa maji na wanaoishi bila umeme, jeshi limetumwa. Wengi wamepata hifadhi kwenye boti lakini kazi hiyoni kubwa kwani maeneo mengi imekumba na mafuriko, hasa Sunamganj au Sylhet, ambapo uwanja wa ndege hauwezi kutumika.

Mvua zenye upepo mkali zimesababisha vifo vya watu 25 na zaidi ya watu milioni nne wamekwama kutokana na mafuriko, polisi imesema leo Jumamosi. Radi imeua watu 21 tangu Ijumaa, huku wengine wanne wakifariki katika maporomoko ya ardhi, kulingana na chanzo kimoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents