Habari

Watu watano wa familia moja wauawa na wasiojulikana Dodoma

Watu watano wa familia moja wamekutwa wakiwa wameuawa nyumbani kwao eneo la Zanka wilayani Bahi mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Mkuu wa Mkoa Dodoma Antony Mtaka pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, Onesmo Lyanga wamefika eneo la tukio usiku wa kuamkia leo ambapo miili ya watu hao imekutwa ikiwa ndani ya nyumba yao walimokuwa wanaishi ikiwa tayari imeharibika.

Waliouawa katika tukio hilo ni Baba, mama, watoto wawili na mjukuu mmoja.

Akizungumza mara baada ya kufika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka amelitaka Jeshi la Polisi mkoani humo kuanza uchunguzi mara moja ili kubaini watu waliohusika kufanya mauaji ya watu hao watano wa familia moja.

Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi kuhusu vifo hivyo, ikiwemo kubaini watekelezaji wa tukio hilo la kikatili.

Source TBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents