Habari

Watu watatu wafariki, saba wajeruhiwa baada ya kupigwa risasi shuleni

Takriban watu watatu, akiwemo mshukiwa wamefariki na wengine saba kujeruhiwa baada ya ufyatuaji risasi katika shule ya sekondari iliyopoSt Louis, Missouri nchini Marekani.

Mtu mwenye silaha aliingia katika shule ya sekondari ya Sanaa-Central Visual & Performing Arts High School, muda mfupi baada ya saa tatu majira ya eneo (13:00 GMT) Jumatatu.

Milango ya shule ilikuwa imefungwa na haikujulikana wazi mara moja ni vipi mshukiwa aliingia ndani.

Walioshuhudia wanasema maisha yalinusurika baada ya silaha ya mwanaume huyo kushindwa kufanya kazi katikati ya shambulizi.

Shule hiyo ya umma ya St Louis inasema polisi “walimzuia haraka” mshambuliaji.

Mshukiwa huyo, aliyetambuliwa na polisi kama mwanafunzi wa zamani wa shule hiyo mwenye umri wa miaka 19, alikabiliana kwa risasi na polisi na baadaye alifariki kutokana na majeraha.

Sababu ya shambulio katika shule hiyo yenye wanafunzi wapatao 400 haijulikani.

Majeruhi saba – wasichana watatu na wavulana wanne – wote hawakuwa na majeraha yanayotishia maisha yao, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents