Watu watatu wamekamatwa Uingereza kuhusishwa na mlipuko wa kigaidi Liverpool

Watatu wakamatwa chini ya Sheria ya Ugaidi baada ya mlipuko wa gari hospitalini jijini Liverpool. Wanaume watatu wamekamatwa chini ya Sheria ya Ugaidi baada ya mtu mmoja kuuawa katika mlipuko wa gari nje ya Hospitali ya Wanawake ya Liverpool.

Teksi iliyokuwa imembeba abiria mmoja ilisimama kabla ya saa 5:00 huku kukiwa na ukimya wa kitaifa wa dakika mbili kwa ajili ya Kumbukumbu ya Jumapili kuanza – na gari hiyo kulipuka.

Abiria huyo aliyetangazwa kufariki katika eneo la tukio bado hajatambuliwa rasmi. Dereva alijeruhiwa na amelazwa hospitalini hali yake inaendelea vizuri.

Wapelelezi kutoka Polisi wa Kukabiliana na Ugaidi Kaskazini Magharibi walisema wanaume watatu – wenye umri wa miaka 29, 26 na 21 – walizuiliwa katika eneo la Kensington jijini humo.

Walisema wanaendelea kupeleleza kuhusu chanzo cha mlipuko huo na wanafanya kazi na Polisi wa Merseyside huku uchunguzi ukiendelea “kwa kasi”.

Kwa mujibu wa BBC Idara ya usalama, MI5, pia inasaidia.

Related Articles

Back to top button