Watumishi waliogushi vyeti wapigwa ‘stop’

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Mohammed Mchengerwa amesisitiza kwamba hakuna mtumishi wa umma aliyeghushi vyeti ataruhusiwa kurudi kazini.

Waziri Mchengerwa akizungumza na wanahabari leo Jijini Arusha

Akizungumza na wanahabari Jijini Arusha, leo Novemba 5, 2021, Waziri amesema kwamba wanaotakiwa kurudi kazini ni wale watumishi waliokuwa wameajiriwa tangu Mei 2004 wakiwa na elimu ya darasa la saba na baadae wakajiendeleza kupata elimu ya kidato cha nne.

Aidha ameeleza kuwa wale walioshindwa kujiendeleza kutokana na muongozo uliotolewa  na serikali ambao idadi yao ni elfu moja na zaidi watatakiwa kulipwa stahiki zao.

Pamoja na hayo, Waziri Mchengerwa  amewakumbusha waajiri wote kukamilisha utekelezaji wa maelekezo hayo kwa haraka na usahihi ili watumishi husika waweze kupata haki zao.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button