
Baadhi ya wanakijiji cha Hokse huko nchini Nepal wamekuwa wakirubuniwa kuuza Figo huku wakidanganywa kuwa zitaota nyingine.
Kijiji hicho miaka kadhaa nyuma kilikuwa maarufu kama kijiji cha “Figo” kwa sababu kila nyumba ilikuwa haikosi mtu aliyeuza figo (Mwenye figo moja).
Madalali wamekuwa wakizunguka kila kona ya kijiji hicho wakiwalaghai wananchi wauze Figo zao japo kwa sasa ni kosa la kisheria kufanya hivyo.
Baadhi Yao wamekuwa wakilalamika kuwa walidanganywa kuwa figo zao zitaota tena na wengine wamepofariki baada tu ya kutolewa Figo hizo kienyeji.
Imeandikwa na Mbanga B.