Habari

Wazee nane watakaosimamia uchaguzi Chadema hawa hapa

 

Katibu Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika ametangaza rasmi kamati ya Waze wastaafu itakayosimamia mikutano ya kitaifa ya uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Mnyika amewataja wazee hao kuwa ni Ahmed Rashid, Alfred Kinyondo, Prof. Azaveli Lwaitama, Wakili Edson Mbogoro, Francis Mushi, Lumuli Kasyupa, Prof. Raymond Mosha na Ruth Mollel.

Kwa mujibu wa Mnyika uteuzi wa wazee hao umefanywa na kamati kuu katika kikao chake cha Januari 11, 2025 kwa kuzingatia kanuni za chama kifungu cha 7.3 juu ya taratibu za kusimamia chaguzi na kupiga kura kipengele cha 7.3.1.

Hata hivyo taarifa hiyo imekuja zikiwa zimepita siku kadhaa mmoja wa wagombea uenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu kuhoji akitaka kujua wazee watakaosimamia uchaguzi huo wa kitaifa na kumtaka Katibu Mkuu atoe orodha yao.

Mgombea mwingine katika nafasi hiyo ni Freeman Mbowe ambaye anatetea kubaki katika nafasi yake baada ya kukiongoza chama hicho kwa miaka 21.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents