HabariSiasa

Waziri ajiuzulu kwa kumkosoa Liz Truss Uingereza 

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella Braverman amejiuzulu jana baada ya kumkosoa vikali Waziri Mkuu Liz Truss, ambaye sasa amepoteza mawaziri wake wawili katika kipindi kisichozidi wiki moja, huku nafasi zao zikichukuliwa na wanasiasa ambao awali hawakumuunga mkono.

Licha ya Truss ambaye yuko madarakani kwa zaidi ya wiki sita tu, kujinadi kama kiongozi asiyekata tamaa, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa chama chake cha kihafidhina kutokana na mpango wake wa uchumi uliozua taharuki katika masoko na kukosolewa vikali kote nchini humo.

Katika mjadala mkali hiyo jana, Wabunge wachache walimtaka ajiuzulu, huku wengine wakijadili ni nani achukue nafasi yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents