HabariSiasa

Waziri Aweso aagiza mkandarasi kufika Kigoma ndani ya saa 24

Waziri wa Maji Mh. Jumaa H. Aweso (Mb) akielekea Buhigwe kwenye ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maji amesimama jimbo la Kigoma Kaskazini na kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Kiganza na Bitale.
Wananchi hao wamewasilisha kero ya kutokuwa na Maji yakutosha katika maeneo yao kutokana Mkandarasi Serengeti Company Limited kushindwa kukamilisha ukarabati wa Mradi wa Maji Mkongoro I kwa wakati.
Mradi wa Mkongoro I unatekelezwa na Taasisi ya Enabel kutoka nchini Ubelgiji na unajengwa na Mkandarasi Serengeti Ltd na kusimamiwa na Mhandisi Mshauri Howard & Humphrey Consulting Ltd kwa gharama ya shilingi bilion 2.8

Aidha, Baada ya kuwasikiliza viongozi wakiongozwa na Mhe Mbunge Asa Makanika, Mh. Waziri ameagiza ndani ya masaa 24 MKandarasi kufika Kigoma na kukutana na RUWASA pamoja na Enabel ofisi ya Mkuu wa Wilaya chini ya usimamizi DC kupitia mkataba kwa kina na kuona kama kuna mapungufu yeyote na kumpatia taarifa ili afanye maamuzi yenye maslahi mapana kwa wananchi.
Waziri Aweso amewaahidi wananchi kuwa ikibainika kuwa kuna tatizo wahusika wote watachukuliwa hatua mara moja.

Mwisho Waziri amewaahidi wananchi kuwa Serikali inasimamia mradi huo na atahakikisha unakamilika haraka iwezekanavyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents