Waziri Bashungwa awapongeza mabingwa wa CECAFA U 23

Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amekutana na mabingwa wa Kombe la CECAFA 2021 U 23 na kuwapongeza kwa kutwaa ubingwa huo ulioletea sifa Taifa.

Mhe. Bashungwa ametoa pongezi hizo jana Agosti 1, 2021 Jijini Dar es Salaam ambapo amesema wizara yake itaendelea kusaidia timu za vijana ili kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu na michezo mingine.

“Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wetu tulikaa chini akatuuliza niwafanyie nini ili kuendeleza michezo tukamwambia tuwe na Mfuko wa kuendeleza michezo nashukuru katika bunge la bajeti la mwaka huu hili swala limepita na mtanufaika kwa mfuko huu” amesema Bashungwa.

Related Articles

Back to top button