Michezo

Waziri Bashungwa: Mchezo wa Simba na Yanga urudiwe na tiketi zirudishwe (+ Video)

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imekutana na kufanya kikao cha mashauriano na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF). Bodi ya Ligi, Baraza la Michezo Nchini (BMT) na Klabu za Simba na Yanga.

Waziri Bashungwa ameagiza kituo cha Kitaifa cha Data kinachosimamia N-card kuwarejeshea tiketi zao kwenye mfumo wa kadi za kuingilia uwanjani Mashabiki wote wa Simba na Yanga 43,947 ili siku ya kurudiwa mechi wakae uwanjani eneo lilelile walilolilipia awali.,

 

Makubaliano yamefikiwa kwenye kikao kilichoongozwa na Waziri Bashungwa kwamba mechi ya Simba na Yanga irudiwe “Wizara inaliacha swala hili katika taratibu za TFF na Bodi ya Ligi ili wakae haraka iwezekanavyo na kutoa tarehe ya kurudiwa kwa mechi hiyo”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents