Habari

Waziri Mhagama ateta na wenyeviti CCM wa mashina Peramiho

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jensita Mhagama Peramiho, amewapongeza Wenyeviti wa Mashina na Kata kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulinda na kukipigania Chama Cha Mapinduzi.

Pongezi hizo amezitoa wakati alipokutana na kufanya vikao na Wenyeviti wa Mashina wa Kata ya Muhukuru Lilahi, Mpitimbi Ndongosi Litapwasi katika ziara yake aliyoifanya tarehe 26 Februari, 2024 Jimboni Peramiho Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.

Amesema Wenyeviti wa Mashina ndio wanaobeba na kusimamia ajenda ya Chama Cha Mapinduzi, na Viongozi wataendelea kuchapa kazi katika utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

“Tunapojiandaa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, hatuna mashaka kwa sababu Viongozi wa mashina wameshaamua Jimbo hili la Peramiho ni la Chama Cha Mapinduzi,” alihimiza.

Aidha amesema kuwa wanafanya hivyo kwa nia ya kuendelea kumshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi kubwa za ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika sekta ya Afya, Barabara, Nishati, Elimu na Utoaji wa pembejeo.

“Tuna kila sababu ya kujivunia mambo mazuri yaliyofanywa na serikali, ili kuimarisha uongozi wa Chama Cha Mapinduzi na tukumbuke kuwa Menyekiti wa Chama wa Taifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawajali nasi hatuna budi kuwajali na kuwaheshimu Wenyeviti wa Mashina” alieleza Waziri Mhagama

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini Ndg. Thomas Masolwa amemshukuru Mhe. Jenista Mhagama kwa kuwathamini na kutembelea Mabalozi wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi ya Shina.

Amesema Mabalozi ni watu muhimu kwa uhai na utendaji wa kazi wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu ndio wanaopokea kero za wananchi.

“Niwaombe Mabalozi muendele kufanya kazi ya kusajili wanachama wapya Ile wale wasio wanachama wawe wanachama wa Chama Cha Mapinduzi,” alisema

Ameongea kusema katika kujenga Chama Mabalozi wahamasishe wanachama katika kulipa Ada ya chama na kufanya mikutano na wananchi kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Awali Katibu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Juma Nambaila amemshukuru nakupongeza Mhe. Jenista kwa kutelekeza Maelekezo ya chama kivitendo kwa kupitia Ofisi za Chama.

“tayari kupokea na kutekeleza maelekezo ya serikali pamoja na maelekezo ya chama, ” alibainisha

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents