Habari

Waziri Mhagama: Endeleeni kulinda amani, na mshikamano wa Taifa letu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuzilinda tunu za umoja wa kitaifa za utulivu, amani na ushirikiano.

Rai hiyo ametoa wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Katika Misa ya kuweka wakfu Askofu wa Jimbo la Njombe Dkt. Eusebius Samwel Kyando iliyofanyika Mkoani Njombe tarehe 14 Januari, 2024.

Waziri amesema kuwa tunu hizo ndizo zinazotambulisha Taifa letu la Tanzania duniani na ulimwenguni kote.

“Tunu hizi zilindwe kwa kuzingatia umuhimu wake, pia Serikali inashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa, tunaomba muendelee kuliombea bila kuchoka ” alifafanua Waziri

Aidha viongozi wa dini mmekua mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa katika hali ya utulivu mstahimilivu na Mhe. Rais amekuwa mstari wa mbele Kati Jambo hilo.

“Niwaombe Sana Viongozi wa dini tuendelee kukemea pale tunapoona kuna viashiria vya watu wachache kuvunja amani, utulivu umoja na mshikamano wa Nchi yetu,” alihimiza

Aidha aliitaka jamii kuungana na Serikali katika kupaza sauti juu ya matendo maovu na hasa mauaji na ukatili wa kijinsia, imani potovu ambazo zinapelekea mauaji na unyanyasaji wa watoto wadogo.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka ameomba viongozi wa dini kwa kushirikiana na serikali kwa pamoja kuunga mkono jitihada zinazofanywa katika sekta ya elimu hasa katika masuala ya lishe kwa wanafunzi mashuleni katika kukabiliana na tatizo la utapiamlo.

“Hii itasaidia kuleta hamasa kuwaandaa watoto kwa kuwapatia lishe Bora ambayo itawasaidia kufanya vizuri katika maisha yao,”Alisema.

Kwa upande wake mmoja wa waumini wa kanisa hilo Bi, Naomi Nzota amesema waumini wa Jimbo la Njombe wamefurahi Sana kwa kupata Askofu Dkt. Eusebius Kyando baada ya Misa wa kuweka wakfu iliyoongozwa na Muasham Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dar es salaam Polcapy Pengo.

“Ameueleza utumishi wa Askofu Dkt. Eusebius Kyando kwamba ni mtumishi, mnyenyekevu mnyoofu na mvumilivu,” alieleza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents