Habari

Waziri Mkuu alivyotinga bandarini na kutoa maagizo haya (+ Video)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa @kassim_m_majaliwa amezitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Serikali Mtandao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam, ameyasema hayo alipotembelea bandari hiyo kujionea utendaji.

“TPA endeleeni kuiimarisha bandari yetu, hii ni sura ya uchumi wa nchi yetu, zungumzeni lugha moja ya uwajibikaji, TRA muwepo maeneo yote yanayohitaji uwepo wenu na muda wote Wateja wetu wahudumiwe ili bandari yetu iendelee kuwa bora, Nchi nyingi zinatutegemea”

“Dosari zote za mfumo wa TANCIS zifanyiwe kazi, mfumo usituharibie, mnapoona kuna madhaifu fanyeni marekebisho ya haraka, tunataka Wateja waingie na kutoka kwa muda mfupi”

Vilevile Waziri Mkuu amemuagiza Kamishna Mkuu wa TRA apeleke Watumishi katika mizani ya TANROADS iliyopo Kurasini Dar es Salam ili kurahisisha ukaguzi wa ‘seal’ pale ambapo magari yamezidisha uzito na yanahitaji kukaguliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents