Siasa

Waziri Mkuu alivyowasimamisha kazi maafisa 6 mkoani Arusha (+ Video)

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa sita wa Jiji la Arusha akiwemo Mkurugenzi wa Jiji hilo, Dkt. John Pima kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za Jiji na tuhuma za kughushi nyaraka.

 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Jumanne, Mei 24, 2022, wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Jiji la Arusha na Halmashauri ya Wilaya ya Arusha kwenye ukumbi wa AICC jijini humo.

Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na Mweka Hazina wa Jiji, Bi. Mariam Shaban Mshana; Bw. Innocent Maduhu (Mchumi), Bw. Alex Daniel Tlehama (Ofisi ya Mchumi, Bw. Nuru Gana Saqwar (Ofisi ya Mchumi) na Bw. Joel Selemani Mtango, Afisa Manunuzi  ambaye alihamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.

Amesema amefikia uamuzi huo kwa  kuwa hawezi kuvumilia kuona fedha za umma zikitumika kinyume na taratibu na akamuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa Mkoa afuatilie masuala hayo hadi ijulikane ni akina nani waliohusika katika ubadhirifu huo.

“ Mdhibit na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG ingia kazini mara moja, tafuta nyaraka zote na wakati huo watumishi hawa watakaa pembeni kupisha uchunguzi hadi kazi hiyo itakapokamilika,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema timu nyingine za uchunguzi zilizokuwa zikifanya kazi kwenye suala hilo ziache mara moja na kuiacha timu maalumu ya uchunguzi ya CAG ifanye kazi yake Timu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents