Habari

Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye arejea CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo Jumatatu Februari 10, 2020 ametangaza kurejea CCM katika ofisi ndogo za chama hicho tawala nchini Tanzania zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Ametangaza uamuzi wake huo mbele ya katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally katika kikao cha baraza la wadhamini kilichoanza leo asubuhi. Dk Bashiru ndio mgeni rasmi katika kikao hicho.

Amerejea CCM takribani miezi miwili tangu alipotangaza kuwa si mwanachama wa Chadema.

Desemba 4, 2019 Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu mwaka 1995 hadi 2005 katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alijivua uanachama wa Chadema na kumuachia ujumbe mwenyekiti wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe.

Alijiondoa Chadema siku chache baada ya kupigiwa kura 48 za hapana kati ya 76 katika uchaguzi wa uenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

Sumaye alieleza kuwa kutokana na yaliyotokea kwenye uchaguzi huo na yeye kuchukua fomu ya kuwania uenyekiti wa Chadema akipambana na Mbowe haoni haja ya kubaki katika chama hicho

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents