Siasa

Waziri mkuu wa Sri Lanka ajiuzulu 

Waziri mkuu wa Sri Lanka Mahinda Rajapaska amejiuzulu Jumatatu kufuatia wiki kadhaa za maandamano yanayomtaka yeye na kaka yake, Rais Gotabaya Rajapaska kujiuzulu kutokana na mzozo mbaya wa kiuchumi.

Maafisa wamesema Waziri Mkuu alituma barua ya kujiuzulu kwa Rais. Waziri mkuu aliandika pia kwenye Twitter kuhusu kujizulu kwake mapema Jumatatu asubuhi.

Kujiuzulu kwa waziri mkuu kumejiri baada ya wafuasi wa chama tawala cha Sri Lanka (SLPP) kuwashambulia Jumatatu waandamanaji wanaoipinga serikali, nje ya afisi za rais mjini Colombo, na kujeruhi watu 200.

Polisi walifyatua gesi ya kutoa machozi na mizinga ya maji na kuweka amri ya kutoka nje usiku ambayo haijulikani lini muda wake utamalizika.

Waandamanaji waliwashtumu viongozi hao ndugu kutoshughulikia ipasavyo kudorora kwa uchumi, hali mbaya ya uchumi ambayo nchi hiyo haijawahi kushuhudia tangu ijipatie uhuru mwaka wa 1948.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents