HabariSiasa

Waziri Ndalichako azungumzia maandalizi siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi DunianiĀ 

Kuelekea siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani Aprili 28, Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kazi, Prof. Joyce Ndalichako ameelezea maandalizi ya maadhimisho hayo yanayofanyika kitaifa Jijini Dodoma.

Katika Mkutano wake na vyombo vya Habari, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, amesema lengo kubwa la maadhimisho haya ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu.

Waziri huyo ameongeza kuwa Tanzania inashiriki katika kampeni ya kidunia kwa kufanya mambo mbali mbali yanayolenga kukuza uelewa wa masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi.

Siku ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi Duniani chimbuko lake ni iliyokuwa siku ya Kimataifa ya kuwakumbuka waliopoteza maisha na kuumia kazini. Siku hiyo ya kuwakumbuka waathirika hao ilianza kuadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1996 huko Marekani katika jiji la Newyork.

Kwa hapa nchini, siku hii ambayo maadhimisho yake huratibiwa na serikali kupitia Taasisi ya OSHA yalianza kuadhimishwa mwaka 2004 ambapo kwa mwaka huu maadhimisho haya yanafanyika kwa mara ya 18.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents