Habari

Waziri Simbachawene ataka Askofu Mwingira ahojiwe kuhusu tuhuma alizotoa

Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. George Simbachawene, ammtaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, kumtafuta na kumhoji Askofu Josephat Mwingira ili kusaidia kupata ukweli zaidi wa tuhuma nzito alizozitoa.

“Nimeona tuhuma zimetamkwa na Askofu Mwingira, tunaendelea kufuatilia, zinapotolewa na kiongozi maarufu, tunapata shida, kwa nini hatoi taarifa, mpaka yametokea, unakaa kimya, unasubiri Krismasi ndio unasema, kama ni kweli, tutahitaji atusaidie atupe ukweli” George Simbachawene

Serikali imeagiza kuhojiwa kwa Askofu Mwingira kwa kile kinachodaiwa kutoa tuhuma za kutaka kuuwawa mara kadhaa na watu wa serikali na wizi wa kura katika chaguzi zilizopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents