Habari
Waziri Ummy, Angellah Kairuki waondolewa kwenye baraza la mawaziri
Katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaondoka katika nafasi za uwaziri Ummy Mwalimu ambaye alikuwa Waziri wa Afya na nafasi yake kuchukuliwa na Jenister Mhagama ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu).
Aidha Waziri mwingine ambaye yupe nje ya baraza hilo ni Angellah Kairuki ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Pindi Chana ambaye alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Katika mabadiliko hayo Kairuki ameteuliwa kuwa mshauri wa Rais huku Ummy hajapewa kazi yoyote.
Written by Janeth Jovin