HabariSiasa

Waziri wa uchumi Japan ajiuzulu

Waziri wa Uchumi wa Japan, Daishiro Yamagiwa,  Jumatatu aliwasilisha barua ya kujiuzulu kutokana na mahusiano yake na kanisa la Unification.

Yamagiwa alikuwa amekabiliwa na ukosoaji mkubwa ambapo hakutoa maelezo kuhusu utatanishi waliyohusika wakiwemo wabunge wa chama kingine na shutuma ambazo zimeikumba serikali ya Waziri Mkuu Fumio Kishida.

Kashfa hii ilitaja miongo kadhaa ya uhusiano wa karibu sana kati ya Waziri Mkuu wa zamani Shinzo Abe ambaye aliuliwa mwezi Julai, wa chama chake tawala cha Liberation Democratic na kanisa la Unification.

Serikali ya Kishida inaunga mkono kushuka kwa viwango vya utenda kazi kwa jinsi ilivyoshughulikia mzozo wa kanisa na kushughulikia mazishi ya Abe.Kishida amesema Jumanne atamtangaza mrithi wa Yamagiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents