Burudani

Wema Sepetu atambulishwa ukweni! “Mimi nikipenda, nimependa”

Malkia wa Filamu Wema Sepetu ambaye kwa sasa anaonekana kuwa na furaha na mpenzi wake msanii wa muziki Whozu, amefunguka kuhusu furaha yake huku akibainisha kwamba tayari ameshatambulishwa ukweni.

Wema aliulizwa na waandishi wa habari kama tayari ameshatambushwa ukweni na yeye akajibu kama tayari ameshatambulishwa.

“Kwani unadhani kwao hawanijui? Muda wote huyo,” alisema Wema.

Kuhusu kuwa na furaha na mahusiano yake alisema “Mimi ni mtu napenda kuonyesha hisia zangu. Mimi nikipenda nimependa, nikichukia nimechukia sipendagi kudanganya. Sasa nadhani kwa muda mrefu sana sijapenda na sijakuwa happy,”

Mara mwisho mrembo huyo kuweka wazi mahusiano yake ni kipindi akiwa kwenye mahusiano na Idris Sultan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents