AfyaHabari

Wengine saba waambukizwa Ebola Uganda

Wizara ya afya nchini Uganda, imethibitisha kuambukizwa kwa watu wengine saba, ugonjwa wa Ebola, baada ya mlipuko kuripotiwa wiki hii katika eneo ma Mubende, Magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha kifo cha mwanamume mwenye umri wa miaka 24.

Watalaam wa afya wanasema aina hii ya virusi, ni Ebola Sudan iliyogunduliwa mwaka 2012.

Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, CDC kinasema Uganda imejiandaa vema kupambana na mlipuko huo, kulingana na Daktari, Ahmed Ogwell Ouma  Mkurugenzi Mkuu wa CDC.

Mataifa jirani kama Kenya na Tanzania, yametangaza umakini katika mipaka yake na Uganda, kuhakikisha kuwa virusi hivyo havisambai.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents