AfyaHabari

WHO: Homa ya Nyani kitisho cha ulimwenguni

Shirika la Afya Duniani WHO limeutangaza mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nyani ambao tayari umeathiri zaidi ya watu 17,000 katika nchi 74 duniani kuwa dharura ya afya ya ulimwengu.

Hiyo ni tahadhari ya juu kabisa inayoweza kutolewa na shirika la WHO kuhusu dharura yoyote ya kiafya ulimwenguni.

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ameuambia mkutano wa waandishi habari mjini Geneva kwamba ameamua kuitangaza Homa ya Nyani kuwa dharura ya kiafya duniani baada ya timu ya wataalamu kushindwa kufikia makubaliano.

Amesema tathmini ya WHO inaonesha kitisho cha Homa ya Nyani duniani bado ni cha wastani isipokuwa barani Ulaya ambako visa vya maambukizi vinaongezeka.

Marekani imeikaribisha hatua hiyo ya WHO katika wakati visa vya ugonjwa huo vinaongezeka huku asilimia 98 ya walioambikizwa ni wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents