Afya

WHO: Janga la Corona ndio dharura kubwa zaidi ya kiafya kuwahi kutokea duniani

Covid 19 ni suala la afya la dharura kubwa kabisa kuwahi kutangazwa duniani na Shirikala afya duniani, WHO, kiongozi wake amesema. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa atakuwa na mkutano na kamati ya dharura ya WHO juma hili kwa ajili ya kufanya tathimini.

Kumekuwa na dharura nyingine zilizowahi kutangazwa kama vile milipuko miwili ya Ebola, Zika, polio na mafua ya nguruwe.

Zaidi ya watu milioni 16 wameripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona tangu mwezi Januari na vifo zaidi ya 650,000.

”Nilipotangaza kuwa hili ni suala la dharura januari 30 kulikuwa na maambukizi chini ya 100 nje ya China, na hakukuwa na ripoti za vifo”. Alisema Dkt Tedros.

Covid 19 imebadili dunia yetu. Imewaleta watu, jumuia na mataifa pamoja, na kuwatawanya.”

Idadi ya maambukizi, aliongeza, imepanda mara mbili zaidi majuma sita yaliyipita.

Ingawa ulimwengu umefanya jitihada kubwa kupambana na virusi, bado kuna ”safari ndefu ngumu mbele yetu,” alisema.

Yanayojiri ulimwenguni:

  • Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa rais wa Marekani Donald Trump, Robert O’Brien amekutwa na virusi vya corona.
  •  Bwana O’Brien ni afisa wa juu katika utawala wa Trump.
  •  Uhispania imesisitiza kuwa watu wapya waliopata maambukizi wametengwa na kuwa nchi iko salama kwa watalii kutembelea, baada ya Uingereza kutangaza masharti mapya kuwataka kukaa karantini kwa siku 14.
  •  Vietinam imefunga mji wake wa pwani wa kitalii, Da Nang, baada ya wakazi 15 wa eneo hilo kuripotiwa kuwa na maambukizi-ripoti ya kwanza nchini humo tangu mwezi Aprili.
  •  Kampuni ya kisayansi ya Moderna nchini Marekani imeanza hatua za mwisho za majaribio ya chanjo muhimu ya virusi vya corona. Watu 30,000 wamejitolea kwenye hatua hii ya tatu nay a mwisho ya majaribio kabla chanjo hiyo haijawasilishwa kwa mamlaka ya udhibiti kwa ajili ya tathimini nap engine kupitishwa kwake.
  •  Ubelgiji imeweka sheria kali kujaribu kuepuka masharti ya kusalia nyumbani kwa mara nyingine kutokana na ongezeko la maambukizi. Kuanzia siku ya Jumatano, raia wa Ubelgiji wataruhusiwa kuwaona ndugu zao si zaidi ya watano nje ya familia zao. Kwa sasa wanauwezo wa kukutana watu wasiozidi 15.

Katika mkutano wa Jumatatu uliofanyika mjini Geneva, WHO pia imesema kuwa kuzuia safari hakuwezi kuwa suluhu ya muda mrefu, na nchi zinapaswa kuchukua hatua zaidi kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona kwa kufuata njia zilizothibitishwa kufanya kazi kama kutocangamana na kuvaa barakoa.

”Haitawezekana kwa nchi kufunga mipaka yao. Uchumi lazima ufunguliwe, watu wanapaswa kufanya kazi, biashara zifunguliwe,” Mkurugenzi wa program wa WHO, Mike Ryan alisema.

Maafisa wa WHO wanatambua hatahivyo, masharti ya kutotoka nje kwa nchi kadhaa zinazokabiliwa na milipuko mipya. WHO yasema haijawahi kupata ‘dharura mbaya ya kiafya’ sawa na corona.

https://www.youtube.com/watch?v=QHrklJATGss&t=1s

https://www.youtube.com/watch?v=OZh3J4VjysE

https://www.youtube.com/watch?v=Njh9NJDgGyA

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents