Habari

WHO yaripoti kushuka kwa idadi ya kesi mpya za Corona Afrika

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaripoti kushuka sana kwa idadi kubwa ya kesi mpya za Covid 19 barani Afrika kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa kirusi kipya cha omicron ambacho kimesambaa kote barani humo miezi miwili iliyopita.

Why other African countries need to guard against South Africa COVID-19  variant

Janga la virusi vya corona limewaathiri takriban watu milioni 10.5 barani Afrika na kuuwa zadi ya 234,000. Maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema kuwa idadi hiyo inaashiria kushuka kwa asilimia 20 kwa kesi za virusi vya corona katika wiki ya Kuelekea Januari 16, na vifo vimeshuka kwa asilimia 8.

Huku wimbi la nne la omicron linaonekana kupata nguvu, mkurugenzi wa kanda ya Afrika katika WHO, Matshidiso Moeti anasema bara hilo bado halijatoka katika janga. Anasema ufuatiliaji zaidi unahitajika kuona kama mwenendo huu unaweza kuhimiliwa.

“Hata hivyo, wakati maeneo manne yameripoti kushuka kwa kesi mpya, tunafuatilia kwa karibu sana huko Afrika Kaskazini, ambako kesi zilikuwa juukwa asilimia 55, na Tunisia na Morocco wote wameona ongezeko kubwa, na kuipiku Afrika Kusini kama nchi ambazo zina kesi nyingi katikat bara hilo,” anasema.

Omicron inambukiza kwa kasi sana na kuchochea ongezeko kubwa la idadi ya kesi. Lakini kuumwa kwake kunaonekana ni kwa kawaida tu kuliko virusi vya awali. Hata hivyo, Moeti anasema bara hilo bado halijarejea katika mwenendo wa kawaida kwasababu ya janga. Anasema hakuna fursa ya kujibweteka.

Anaonya kuwa mawimbi ya janga hayaepukiki ili mradi virusi vinaendelea kusambaa. Anaelezea kuwa Afrika bado iko katika mazingira hatarishi kwasababu ya fursa isiyo sawa kwa chanjo za kuokoa maisha. Anasema Afrika inakabiliwa na vikwazo katika kupata fursa ya matibabu kamili ya Covid 19.

WHO imeidhinisha matibabu ya aina 11 ambayo yanaweza kutumia kutibu Covid 19. Hivi sasa inaangalia data kuhusu dawa mbili za kunywa, ambazo zimeonyesha matokeo ya kutia moyo katika kupunguza hatari ya kulazwa hospitali kwa baadhi ya wagonjwa.

Mkurugenzi wa WHO Afrika, Moeti anasema anahofia bara la Afrika kwa mara nyingine tena huenda likapoteza fursa ya mafanikio kwa matibabu hayo kwasababu ya upatikanaji wake na gharama kubwa. Kwa mfano, anaelezea matibabu ya aina mbili ambayo. Yanagharimu kati ya dola 550 na 1,200 kwa dozi moja.

“Ukosefu wa usawa ambao umeiacha Afrika nyuma katika foleni ya chanjo lazima usirejewe tena katika matibabu ya kuokoa maisha. Fursa ya ulimwengu kutambua ugonjwa, chanjo na matibabu kutafungua njia kwa kufikia katika kumaliza janga hili,” anasema Moeti.

Moeti anayaonya mataifa kujitayarisha wimbi jingine la maambukizi, pengine vrusi hatari zaidi vya corona. Anasema virusi vya corona vitaendelea kuzaliana na kuwa tishio linaloendelea kwa mataifa kama hayana usambazaji wenye usawa wa chanjo.

Source: Voice Of America

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents