Technology
Will.i.am azindua smartwatch mpya zinazopiga simu zenyewe!
Pamoja na kwamba smartwatch zinaweza kufanya mambo mengi, zinakosolewa vikali kwa kutegemea simu ili kufanya kazi zingine.
Pengine hili limepata ufumbuzi baada ya muimbaji na mjasiriamali, Will.i.am kuzindua smartwatch zake zinazoweza kupiga simu au kutuma sms bila kuunganishwa na simu.
Anaamini kuwa ubinifu wake utaleta mapinduzi. Kiongozi huyo wa kund la The Black Eyed Peas alizindua saa hizo ziitwazo ‘dial’ wikiendi jijiji London.
Saa hizo zinajitegemea zenyewe tofauti na Apple Watch. Hii ni kwasababu saa hiyo ina Wi-Fi na SIM card yake yenyewe hivyo kuiwezesha kuunganisha na internet ya kawaida au ya kwenye simu.
Zitaingia sokoni mwezi April.