Wimbo wa Stamina na Profesor Jay ‘BABA’ ndio wimbo bora 2021 ? ujumbe wake wawaliza wengi (+ Video)

BRABD NEW VIDEO: Moja ya ngoma bora zilizotoka mwanzoni mwa mwaka 2021 ni huu wa @staminashorwebwenzi #BABA na huenda wimbo huu ukaendelea kufanya vizuri katika masikio ya Watanzania wengi.

Ujumbe mzito uliopo kwenye wimbo huu wa @staminashorwebwenzi aliowashirikisha Mkongwe @professorjaytz pamoja na @onesix1 ndio unafanya watu kujiuliza na kujipa majibu kuwa huenda ukawa wimbo bora uliotoka mwaka 2021.

Katika jamii za Kitanzania ujumbe huu unawahusu wengi sana na mara nyingine unaweza ukawa unamtupia lawama Baba/Mama lakini hujui kilichopo nyuma ya pazia, kupitia comment za mashabiki ambazo wanaziandika chini ya video hiyo wameelza jinsi wimbo huo ulivyowatoa amchozi.
Usikilize kwa makini halafu toa maoni yako na tuambie unampa asilimia ngapi Stamini kwa ngoma hii….?

Related Articles

Back to top button
Close